Programu zetu

Event 1

MAFUNZO NA ELIMU YA KILIMO HAI

Tunatoa mafunzo, elimu na hamasa kwa vijana na jamii kujikita kwenye kilimo hai cha mboga mboga na matunda katika maeneo mbalimbali ya mjini na vijijini.Lengo kuu la program hii ni kuongeza ajira kwa vijana wa mjini na vijijini kwa kutumia maeneo yanayowazunguka kulima matunda na mboga mboga zisizotumia malighafi za viwandani, kubadili mtazamo na fikra za vijana na jamii kuwa kilimo ni shughuli muhimu kwa kila mwanadamu na sio kwa walishindwa maisha kama wanajamii wanavyofikiri kuhusu kilimo, kuhamasisha jamii kujikita kwenye kilimo hai ambacho ni rafiki kwa mazingira, kulinda afya ya mlaji na utumia gharama nafuu kutumia malighafi zinazowanguka kwenye mazingira wanayoishi, Kuhmasisha vijana kutumia fursa ya kilimo hai kama sehemu ya ajira ya kuingiza kipato na kukuza uchumi wa familiai. Katika utekelezaji wa programu hizi Care Youth Foundation ushirikiana na wadau na mashirika mbalimbali ndani na nje katika kuhakikisha vijana na jamii wananufaika na programu hizi

Event 2

UFUGAJI

Care Youth Foundation inatoa elimu na mafunzo ya ufugaji wa kuku wa kienyeji na kisasa, Bata, sungura, nyuki na njiwa ili kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za ufugaji kwenye maeneo yao ambapo wanaweza kutumia eneo dogo au kubwa kujipatia mahitaji muhimu ya chakula na kuingiza kipato. Dhumuni la elimu hii ni kuongeza wigo kwa vijana kutambua fursa zilizopo kwenye jamii na kuzitumia kuinua uchumi. Care Youth Foundation kupitia elimu ya ufugaji inawaelekeza vijana mbinu rafiki za ufugaji na mitaji anzia.

Event 2

UJASIRIAMALI

Ujariamali ni jambo muhimu katika maisha kwani uongeza nafasi kubwa kwa vijana kuchagua aina ya ujasiamali kulingana na mazingira wanayoishi. Care Youth Foundation kwa kutambua umuhimu wa fursa ya ujasiriamali kwa vijana inawajengea uwezo na mbinu mbali mbali za kijasiriamali kama vile kutambua aina ya ujasiriamali na mazingira, vyanzo vya ujasiriamali, jinsi ya kupata mitaji, uendeshaji wa ujasiamali, ushiriki wa jinsia katika shughuli za ujasiriamali na utunzaji wa fedha zitokanazo na ujasiriamali. Mafunzo haya ufanyika kwa nadharia na vitendo ili kwawezesha vijana kupata uelewa zaidi. Baadhi ya mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa na Care Youth Foundation ni Ushonaji wa nguo, uchakataji wa ngozi, utengenezaji wa sabuni na bidhaa za shanga, utengenezaji wa viatu, usindikaji wa bidhaa za shambani na uzalishaji wa mkaa mbadala. Asasi inahamasisha vijana kuunda vikundi vya kijasiriamali ili kuimarisha umoja katika uzalishaji na kuvutia wadau wa uwekezaji.

Event 2

MAZINGIRA

Care Youth Foundation inafanya uhamasishaji na utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira katika jamii kama vile kutenegenza vitalu vya miche ya miti ya matunda, kupanda miti sehemu za wazi na maeneo wanayoishi, kutembelea shule za msingi, sekondari na vyuo kutoa elemu ya mazingira..

Event 2

ELIMU YA JINSIA NA AFYA

Kuelimisha jamii hasa vijana juu ya jinsia, Ukatili wa kijinsia, Mimba na Ndoa za Utotoni pamoja na UKIMWI. Care Youth Foundation inaijengea jamii uelewa wa kukabiliana na changamoto mbali mbali za afya na jinsia zinazokwamisha maendeleo nyuma kama vile ushiriki mdogo wa jinsia katika shughuli za uchumi, ongezeko la maambukizi ya UKIMWI, vijana kupoteza maisha kupitia vifo vya ajali, matumizi ya madawa ya kulevya yanayodhhoofisha mwili na kupunguza nguvu kazi katika jamii na kusababisha ongezeko la watoto yatima na wahitaji wengi. Vijana kutozingatia afya ya uzazi na haki na kupelekea vijana kupata magonjwa ambukizi, kupata mimba zisizotarajiwa na kutoshiriki shughuli za kijamii

Event 2

KUTOA KWA JAMII

Care Youth Foundation ushiriki na kuhamasisha kutoa na kujitolea kwa jamii kama vile kutembelea vituo vya watu wenye mahitaji maalum, kushiriki shughuli za ujenzi wa taifa kama vile ujenzi wa shule za umma, hospitali na miundo mbinu ya umma, kuchangia na kushiriki shughuli za kimaendeleo kama vile makongamano na sikukuu mbalimbali za kitaifa na kimataifa. Programu hii ni ya kujitolea kwa kuhusisha na kushirikisha wanachama wa asasi na nije ya asasi ya Care Youth Foundation